MAUDHUI KATIKA MAPAMBAMZUKO YA MCHWEO (TAASUBI YA KIUME)
MAUDHUI KATIKA MAPAMBAMZUKO YA MCHWEO (TAASUBI YA KIUME)
TAASUBI YA KIUME
• Luka anampiga mkewe Lilia kwa ngumi, teke, kofi na hata kumfokea. Mara ya mwisho ilikuwa teke lililompata tumboni sawasawa, asiweze kujinyoosha kwa siku mbili kwa sababu ya maumivu makali.(uk l)
• Luka anampiga mkewe Lilia kwa kisingizio kuwa chakula hakikukolea chumvi. Uso wa Lilia umejaa kovu badala ya ngozi nyororo, vidu na tabasamu ya daima kutokana na vipigo vya mumewe.(uk l)
• Baada ya kuanza uzinzi na hawara zake, Luka anakuwa mkali kwa mkewe. Kucheka kwake kunakuwa nadra kama mwezi kupatwa; anageuka kuwa mzigo moto -habebeki kamwe.(uk l)
• Baada ya kifo cha babake Lilia, mumewe Luka anamshinikiza kuacha kazi kwa madai kuwa anamhitaji kudhibiti fedha za kanisa. (uk 4)
• Baada ya kuacha kazi Lilia anasukumiwa kazi za utawa-kukaa nyumbani kupokea utiriri wa wageni wa kanisa(wageni wa mumewe)(uk 4)
• Kazi za Lilia zinakuwa kuonekana ila si kunena.Wake hawana usemi nyumbani.(uk 5)
• Ushauri wa wanawake unapuuzwa. Lilia anambembeleza mumewe asiingilie siasa ila Luka alishatunga na akishatunga habadili.(uk 5)
2021 KCSE PAPERS FREE DOWNLOAD ALL SUBJECTS
Nambale Joint Mock Examinations
Bungoma Diocese Post Mock 2022 Free Papers And Marking Schemes
WISDOM PRE-MOCK 2021 PAPERS AND MARKING SCHEMES FREE
• Luka analiuza kanisa lao pasi na kummshauri wala kumwuliza mkewe Lilia. Lilia anatanabahi kanisa limeuzwa.(uk 5)
• Badala ya Lilia kurithi mali/biashara ya babake (kanisa), ni mumewe ndiye anayelirithi. Kanisa hili lilianzishwa na babake Lilia.
• Ni jukumu la wanawake kunyamazia maovu kwenye ndoa ili kudumisha amani kwenye ndoa zao.(uk 5)
• Wanawake wanatumiwa na waume zao ili kusawiri hadhi bora kifamilia. Luka anamwandama Lilia ubavuni mwake kama taswira ya kiongozi anayethamini ndoa na familia yake. Lengo lake ni kuchaguliwa na raia.(uk 5)
• Lilia angekataa kuandamana na mumewe anatusiwa kuwa mnene kama nguruwe na kuwa hana kazi maalumu.(uk 5)
• Wanawake kama Lilia wakikataa kutekeleza haja za waume zao hutishiwa. Lilia anatishiwa kuwa wanawake ni wengi.(uk 5)
• Wanawake wanatumiwa kama vyombo vya starehe. Luka ana hawara tele licha ya kuwa na mke.(UK 5)
• Wanawake huwangoja ‘.vaurne zao kurejea nyumbani kabla hawajalala.Lilia anamgojea Luka usiku kucha hadi anapoteza ujauzito.(UK 5)
• Luka anamtenga Lilia kuishi kijijini ili kuwahakikishia raia wapiga kura kuwa Gavana yu karibu.(UK 5)
• Wanawake wanahita)i miadi kabla hawajawatembelea waume zao. Luka anamfahamisha Lilia kuwasiliana na mhazili wake akapewe miadi ndiposa amtembelee.(uk 6)
• Wanawake wananyimwa nafasi ya kutoka nyumbani. Luka anamtisha Lilia kuwa kitoka nje ya lango atajua kilichomtoa kanga manyoya shingoni. Wanawake wanatengwa na marafiki zao. Lilia amejitenga na marafiki take maanake kila wakimtembelea mumewe anajua na kuishia kumpa kichapo.(uk 6)
• Nanawake hawafai kuwashtaki waume zao. Lilia anapothubutu kusema angemshtaki mumcwe inakuwa kama kuchokoza nyuki, anapigwa.(uk 6)
• Wanawake hawafai kuulizia hawara za waume zao. Lilia anapouliza mwanamke aliyemwona ameandamana na mumewe kwenye vyombo vya habari, alijibiwa kwa kipigo kilichomlaza kitandani siku mbili.(uk 7)
• Lilia anapigwa kipigo cha kifo kwa kujaribu kuripoti mumewe kwenye kituo cha polisi. Japo hakumripoti, kuonekana kwenye kituo cha polisi ndicho kinachomletea vipigo.(uk 7)