MWONGOZO WA MAPAMBAMZUKO YA MCHWEO (JALADA)
MWONGOZO WA MAPAMBAMZUKO YA MCHWEO (JALADA)
JALADA
Jalada ni sehemu iliyoko juu ya kitabu hasa huwa ngumu na mambo yaliyo muhtasari wa kile msomaji anataraji ndani. Jalada huwa kuwili yaani, jalada la mbele na la nyuma. Kunavyo vipengele muhimu hasa rangi za michoro na maandishi.
Jalada lina anwani Mapambazuko ya Machweo na hadithi nyingine. Chini ya anwani hii kuna picha za watu watatu wazima na za watoto wawili. Picha ya mtu wa kwanza aliyevalia suti ya kijani kibichi, tai na miwani na kuonekana kuingia gari jekundu inasawiri tajiri aliyekuja kumtuza mzee Makucha.
Picha ya pili ya mwanaume anayeonekana kufurahi na pesa mkononi inamsawiri mhusika mzee Makucha ambaye amefurahia kupokea tuzo baada ya kuwaokoa watoto wadogo waliokuwa wakifanya kazi migodini mwa mzee Makutwa.
Picha ya tatu ya mwanamke anayefurahi pamoja na mwanaume wa pili inamsawiri Bi.Macheo, mkewe mzee Makucha, anayejiunga naye kufurahia tuzo aliyopewa mumewe.
Bungoma Diocese Post Mock 2022 Free Papers And Marking Schemes
WISDOM PRE-MOCK 2021 PAPERS AND MARKING SCHEMES FREE
Nyuma yao kuna nyumba ambayo ina mabati yaliyozeeka inayoashiria hali ngumu ya kiuchumi ambayo familia ya mzee Makucha imepitia baada ya kufutwa kazi na Shirika la Reli.
Aidha, kuna picha ya watoto wawili: msichana na mvulana wanaofanya kazi ngumu.
Msichana amebeba besini na mvulana ameinama kupakuwa mchanga kwenye kijiko.
Wanaonekana wamechafuka. Picha hii inarejelea watoto wanaofanya kazi ngumu katika mgodi wa mzee Makutwa wanaookolewa baadaye na mzee Makucha.
Chini ya jalada upande wa kulia kuna meza na kiti. Juu ya meza kuna bidhaa mbalimbali za kuuzwa kuonyesha biashara iliyokuwa ikifanywa na familia ya mzee Makucha.
Pia kuna mwanga wa jua unaowamulika mzee Makucha, Bi. Mchewa na wale watoto wawili.
Mwangaza huu ni ishara ya matumaini au fikra endelevu katika jamii. Unaweza kurejelea kitendo cha mzee Makucha kuwaokoa watoto waliokuwa wakifanya kazi migodini au tuzo anayopata mzee Makucha kwa kitendo hicho cha kuwaokoa watoto.