MWONGOZO WA MAPAMBAMZUKO YA MCHWEO (MUHTASARI)
MWONGOZO WA MAPAMBAMZUKO YA MCHWEO (MUHTASARI)
1. FADHILA ZA PUNDA – (Rachel Wangari)
• Lilia ni msichana mcha Mungu. Amelelewa katika mandhari ya dini na babake, pastor Lee Imani, ambaye ndiye mhubiri mkuu kanisani mwao. Mamake Lilia ameshafariki katika ajali ya barabarani.
• Kanisani, anajitokeza Luka ambaye ni mvulana maskini ila ana sauti nzuri ya kuimba, kitu ambacho kinamvutia sana Lilia. Lilia anamrai babake kumsaidia Luka. Luka anapelekwa shuleni na mamake anapewa kibarua cha kunadhifisha mazingira kanisani kwa babake Lilia.
• Miaka inavyosonga ndivyo babake Lilia anaingiwa na hofu kuhusu mahusiano kati ya bintiye na Luka. Hivyo, anamtuma Luka kusomea sehemu nyingine ya nchi huku akiishi kwa mhubiri mwenzake. Badala ya urafiki kufifia, unageuka na kuwa mapenzi. Baadaye, Luka na Lilia wanaishia kusoma katika Chuo kimoja na hatimaye Lilia anamrai babake amruhusu kupendana na Luka.
• Baada ya masomo yao, Luka anapewa majukumu ya uhubiri kanisani na ruhusa ya kumuoa bintiye mhubiri mkuu. Wanafunga ndoa na Luka anakuwa maarufu katika kazi yake kanisani mpaka watu kutoka nchi mbalimbali wanakuja kanisani humo kwa ajili ya miujiza aliyoifanya.
• Baada ya babake Lilia kufariki, Luka anatwaa uongozi wa kanisa kwa muda kabla ya kumwachisha mkewe kazi katika benki ili kuwa karibu zaidi kwa utumishi wa kanisa. Ndoa yao inaanza kuwa na matatizo
• Luka anapoamua kuacha kazi ya uhubiri na kuwa mwanasiasa. Wakati huu, mkewe ashakuwa mke wa nyumbani, anatawishwa. Luka, ambaye alikuwa mhubiri wa injiii, anageuka kuwa mwanasiasa na mume katili kwa mkewe, mkombozi wake wa utotoni.
Ukatili wake unadhihirika tangu mwanzo mpaka kufikia wakati anamuumiza sona. Lilia anachukuliwa na mama mkwe wake, Luka, na kupelekwa hospitatini kupata matibabu kwa maumivu anayopata kutokana na kichapo cha mumewe. Wakati huo huo, Luka anapata ajali mbaya ya barabarani na kuumia sana. Anatozwa katika chumba kimoja na mkewe.
Baadaye, kwamba Luka huenda asiweze kutembea tena kutokana na athari za ajali. Kimada wake anapopata taarifa hii, anapotea kabisa asirudi hospitalini kumjulia hali. Inakuwa kwamba kwa kumtetekeza mkewe, Luka anaacha mbachawe kwa msala upitao,Mandhari ya hadithi Mandhari ya hadithi hii ni mashamboni na pia mjini. Lilia anakutana na Luka mora ya kwanza mashambani anapokuja kanisani. Wanaendelea kuishi huko. wakati mmoja Luko akienda kusomeo katika sehemu tofauti yo nchi. Hata hivyo, Luka anapokuwo Gavana anaishi mbali na nyumbani, mjini.